TAARIFA ZA KAMUSI


TAARIFA ZA KAMUSI

Kanusi hua na taarifa mbalimbali miongoni mwa taarifa za kamusi ni kama zifuatazo
KITOMEO

Kitomeo ni neno linaloorodheshwa katika kamusi ili litolewe maana zake pamoja na taarifa nyenginezo.Katika kamusi vidahizo vinaorodheshwa katika chapa iliyokozeshwa wino mzito. Mfano Ardhi nm1; nchi kavu,udongo, duniani

Fuska.nm; tabiya mbaya hasa ya uasharati

VISAWE Visawe ni maneno yenye maana sawa yaani neon jengine linaloweza kutumiwa badala  ya neno la kwanza. Mfano runinga kisawe chake ni televisheni, tembo kisawe chake ni ndovu ,nyanya kisawe chake ni bibi na kadhalika .Hivyo maneno haya yenye maana sawa au yanayokaribianasana kimaana yanaonyesha utajiri wa lugha Fulani na kuwezasha kuremba sentensi mazungumzo na maandishiviwe na uzuri wa kifasihi

TAHAJIA YA MAMNENO

Tahajia ni uwasilishaji wa sauti kwa herufi katika maandishi kufuatana na mwendelezo wa manenouliokubaliwa.maneno katika kamusi yanaandikwa kwa kufuatanana tahajia sanifu ,kwa yale maneno yenye tahajia zaidi ya moja katika kamusi tahajia zote hua zinaoneshwa.

MAANA YA MANENO

Kamusi huonesha maana za maneno ,maana hizo zinaeleezwa kwa kutoa fasili (maelezo)pamoja na maneno mengine yenye maana sawa au zinazokaribiana yaani sinonimu, kimpanglio fasili hutangulia na sinonimu hufuata.

MATUMIZI YA MANENO

Kamusi huonesha matumizi mbali mbali ya maneno,kwa kawaida maneno mengi ya lugha hutumiwa katika Nyanja mbali mbali hata hivyo kuna baadhi ya maneno hutumika zaidi katika maeneo  Fulani kama vili dini,fizikia ,bayolojia ,ushairi na sarufimaneno kama haya hupewa alama maalumkuonesha maneno yanayo tumika zaidi.

No comments:

Post a Comment

MATUMIZI YA KAMUSI

MATUMIZI YA KAMUSI NI MUHIMU SANA KWA WATUMIAJI WA LUGHA HUSIKA KWA SABABU HUKUZA LUGHA YA MTUMIAJI