MUUNDO WA KAMUSI


MUUNDO WA KAMUSI


 Kamusi imegawanyika katika sehemu kuu tatu,  nazo ni utangulizi, matini ya kamusi,  na sherehe ya kamusi.

Utangulizi wa kamusi

Hii ni sehemu ya mwanzo ya kamusi ambayo hutangulia matini yenyewe ya kamusi.utangulizi hujumuisha muhtasari wa sarufi ya lugha yenyewe pamoja na maelezo ya namna ya kutumia kamusi .Utangulizi huonesha pia vifupisho vilivyotumika ndani ya kamusi na maana zake.

Mtini ya kamusi.
Hii ni sehemu yenye vidahizo vyote vya kamusi husika kuanzia herufi ya alfabeti “A”hadi “Z”.vidahizo vyote huorodheshwa hapa na kufafanuliwa .Taarifa mbalimbali za kiisimu hufafanuliwa hapa

Sherehe ya kamusi

Sehemu hii ya kamusi huingiza baadhi ya taarifa za ziada zenye masaada kwa mtumiaji wa kamusi.Taarifa zianazoingizwa katika sehemu hii ni kama vile,

·         Majina ya nchi mbali mbali

·         Vyeo vya kijeshi

·         Vipimo mbali mbali vya urefu ,ujazo,ukubwa n.k

No comments:

Post a Comment

MATUMIZI YA KAMUSI

MATUMIZI YA KAMUSI NI MUHIMU SANA KWA WATUMIAJI WA LUGHA HUSIKA KWA SABABU HUKUZA LUGHA YA MTUMIAJI