Kwa kuzingatia kigezo chaa lugha kuna aina tatu za kamusi.
Kamusi wahidia
Hii ni aina ya kamusi iliyoandikwa kwa kutunia lugha moja tu, na inalengwa kwa wazungumzaji wazawa wa lugha hiyo. Wakati mwengine huwafaa wanao jifunza lugha hiyo kama lugha ya pili au lugha ya kigeni . Viadahizo vya kamusi wahidiya na maelezo ya vidahizo hivyo huwa katika lugha moja. Mfano wa kamusi wahidia ni
Kamusi thaniya
Hii ni aina ya kamusi iliyoandikwa kwa lugha mbili. Katika kamusi ya aina hii vidahizo huandikwa kwa lugha moja (lugha chanzi) na maelezo ya maana mbayo aghalabu hua neno moja yaani visawe ,huandikwa kwa lugha nyengine (ligha lengwa ) lengo la kamusi thaniya ni kumsaidia mtu anaefahamu lugha moja kati ya zilizotumiwa kujifunza lugha nyengine, kuelewa matini anazosoma ambazo zimeandikwa katika lugha za vidahizo vya kamusi na kumsaidia kujieleza vizuri hasa anapoandika katika lugha lengwa. Mfano wa kamusi thaniya ni kamusi ya kiswahili kiingereza na english swahili dictionary
Kamusi mahuluti
Hii ni aina ya kamusi yenye lugha zaidi ya mbili. Ni kamusi iliyoandikwa kwa lugha nyimgi, Vidahizo vya kamusi mahuluti hapatiwa visawe kutoka katika lugha mbali mbali mfano wa kamusi mahuluti nik kamusi ya kifaransa- kingereza- kiswahil
No comments:
Post a Comment